Katika kuendeleza mradi wa kupanda miti kwenye barabara za mji mtukufu wa Karbala, idara ya upandaji wa miti chini ya kitengo cha utumishi katika Atabatu Abbasiyya imeanza kazi ya kupanda miti kwenye barabara iliyopo jirani na haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), mkabala na mlango wa Amiir (Baabu-Kafu) kupitia barabara ya Alqamiy hadi mwisho wake.
Miti iliyo pandwa ni aina ya Akasiya ambayo miche yake ilioteshwa kwenye vitalu vya Alkafeel chini ya Atabatu Abbasiyya, miti hiyo imepandwa kwa wingi jirani na malalo tukufu kuanzia Baabu-Kafu kupitia barabara ya Alqamiy hadi mwisho wake.
Fahamu kua mti wa Akasiya unakivuli na mauwa mazuri nayo ni mingi katika maeneo ya tambalale, ipo sehemu mbalimbali duniani, ardhi na hali ya hewa ya Iraq ni nzuri kwa mti huo, ndipo ukapandwa katika vitalu vya Alkafeel na wao ndio wasambazaji wakuu wa mti huo hapa Iraq.
Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia shamba boy wake inafanya kazi ya kupanda miti kwenye barabara za mji wa bwana wa mashahidi na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) Karbala tukufu, na kuufanya uwe na muonekano wa kijani kibichi kwa kiasi ambacho utaingiza furaha katika nafsi ya zaairu.