Kuhitimisha mashindano ya kuhifadhi na kusoma Quráni kwa wanafunzi wa sekondari (upili) na kamati ya maandalizi yatangaza majina ya washindi.

Maoni katika picha
Kituo cha kitaifa cha maarifa ya Quráni tukufu chini ya uongozi wa wakfu Shia kwa kushirikiana na Maahadi ya Quráni katika Atabatu Abbasiyya, wameratibu mashindano ya kitaifa ya pili ya kuhifadhi na kusoma Quráni tukufu kwa wanafunzi wa sekondari (upili) kama sehemu ya kujiandaa na mashindano ya kimataifa.

Mashindano hayo yamefanyika ndani ya ukumbi wa jengo la Alqami chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, yalifunguliwa kwa Quráni iliyo somwa na Faisal Matwar, ukafuatia ujumbe kutoka kwa rais wa ugeni Ustadh Sami Ghalawi, Ameishukuru Atabatu Abbasiyya kupitia Maahadi ya Quráni kwa ushirikiano wake katika kuendesha mashindano haya, kama alivyo washukuru washiriki wote na akawatakia mafanikio mema.

Mashindano yalikua na vikao viwili, kikao cha kwanza kilihusu kuhifadhi Quráni na kilianza saa tatu asubuhi, na kikao cha pili kilianza baada ya Adhuhuri na kilihusu usomaji wa Quráni, jumla ya washiriki wa usomaji na kuhifadhi ni zaidi ya thelathini, chini ya usimamizi wa kamati ya majaji iliyo undwa na:

Ustadh Haafidh Makkiy Saadi jaji wa ubora wa hifdhu.

Ustadh Haafidh Ali Muhammad jaji wa ubora wa hifdhu.

Ustadh Ali Abudi Twaaiy jaji wa hukumu za tajwidi.

Ustadh Mustafa Ghalibiy jaji wa sauti.

Ustadh Faisal Matwar jaji wa naghma.

Mwisho wa mashindano yakatangazwa majina ya washindi wa hifdhu na usomaji kama ifuatavyo:

Washindi wa hifdhu:

Mshindi wa kwanza: Haafidh Sefu Mustafa Latifu.

Mshindi wa pili: Haafidh Mussa Akram Naiis.

Mshindi wa tatu: Ali Abbasi Hussein.

Washindi wa usomaji ni:

Mshindi wa kwanza: Hussein Haadi Ismail.

Mshindi wa pili: Muqtada Hussein Inadi.

Mshindi wa tatu: Daniel Karim Ghadhbani.

Mwisho washiriki wote wakapewa vyeti, na kituo cha kitaifa cha maarifa ya Quráni kikatoa pongezi kubwa kwa washindi na wahudhuriaji wote kwa ujumla.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: