Idara ya usimamizi wa haram tukufu yawajengea uwezo watumishi wake.

Maoni katika picha
Miongoni mwa malengo ya Atabatu Abbasiyya ni kuboresha huduma katika malalo tukufu, kulingana na kitengo cha kazi ya kila mtumishi, ili kutimiza lengo hilo hufanya semina za kuwajengea uwezo watumishi wake kila baada ya muda fulani, ndani na nje ya Ataba tukufu, yote ikiwa ni njia ya kuboresha uwezo wa wahudumu katika utoaji wa huduma sambamba na kuboresha elimu zao.

Idara ya usimamizi wa haram tukufu inawapa semina watumishi wake inayo lenga kuboresha utendaji wa majukumu yao.

Semina hiyo inafanywa kwa kushirikiana na shirika la kuendeleza uwezo wa binaadamu, ambalo ni miongoni mwa mashirika yenye uwezo mkubwa na uzowefu wa kuendeleza uwezo wa mtu, imesimamiwa na Ustadh Azhar Rikabi ambaye ni mkuu wa shirika, na amesema kua: “Semina hii inakusudia kuboresha utendani wa mtumishi katika kutoa huduma, mada zilizo fundishwa sio tu zinalenga mwenendo wa watumishi bali hadi fikra zao pia, tumebaini wanahisia kubwa ya kupenda maendeleo, kwani wanakanuni ya msingi ya jambo hilo”.

Washiriki wa semina wamesema kua: “Semina hii imetupa upeo mkubwa, katika upande wa kufanya kazi na kuamiliana na mazuwaru sanjari na familia, faida ya pili; imekua ni sehemu ya kuonyesha uwezo tulionao na kuboresha utendaji wa kazi zetu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: