Maahadi ya Quráni tukufu/ tawi la Baabil chini ya Atabatu Abbasiyya imefanya vikao kadhaa vya usomaji wa Quráni na kuelekeza thawabu kwa mashahidi wa vita ya islahi, waliotoka kuandamana kwa ajili ya kudai maisha bora kabla ya kujitolea roho zao katika ushindi wa vita kubwa ya islahi, vita ambayo Marjaa ameiita kua ni vita kali na ngumu kushinda vita ya ugaidi.
Vikao vya usomaji wa Quráni vimefanyika ndani ya kituo cha Maahadi katika mkoa wa Baabil, na kwenye misikiti na husseiniyya huku vikihudhuriwa na idadi kubwa ya wakazi, hiyo ni kwa ajili ya kuheshimu roho zao na damu iliyo mwagika kwa aili ya kutafuta islahi.
Kumbuka kua Maahadi ya Quráni tukufu kupitia matawi yake mbalimbali inaendelea kuwakumbuka mashahidi wote wa taifa hili kwa kufanya visomo vya Quráni na kuelekeza thawabu kwa mashahidi hao watukufu.