Katika lango la jengo la Shekh Kuleini pametengenezwa mfano wa kiriba cha Abulfadhil Abbasi (a.s).

Maoni katika picha
Mafundi wanaofanya kazi katika jengo la Shekh Kuleini chini ya Atabatu Abbasiyya, lililopo barabara ya Bagdad – Karbala, wametengeneza mfano wa kiriba cha Abulfadhil Abbasi (a.s) katikati ya muelekeo wa lango kuu, hiyo ni miongoni mwa kazi nyingi zinazo fanywa na mafundi hao kwa ajili ya kuweka muonekano mzuri wa jengo hilo utakao furahisha macho ya mazuwaru.

Kiongozi wa jengo hilo Ustadh Ali Mahdi Abbasi Swafi ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Kazi hii ni miongoni mwa mfululizo wa kazi za mafundi wanaofanya kazi kwenye jengo hilo, inalenga kuweka muonekano mzuri utakao wafurahisha waangaliaji, nayo ni kutengeneza kiriba kinacho fanana na kile alichokua nacho Abulfadhil Abbasi (a.s) ambacho kinatoa maji, huku kikiwa kimekaa juu ya kubba ndogondogo za duara 16 kikiwa na upana wa (mita 2) na urefu wa (mt 2 na sm 20), kikizungukwa na nguzo nne zilizo pambwa maua ya kawaida na taa za rangi”.

Kumbuka kua jengo la Shekh Kuleini lipo katika barabara ya (Bagdad – Karbala) umbali wa (km 6) kutoka katikati ya mji wa Karbala, lilijengwa kwa ajili ya kutoa huduma kwa mazuwaru wa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), hususan katika ziara zinazo hudhuriwa na mamilioni ya watu, kama vile ziara ya Arubaini na nusu ya mwezi wa Shabani, milango ya jengo hilo ipo wazi kila siku mwaka mzima sambamba na kufanywa harakati nyingi na Atabatu Abbasiyya katika jengo hilo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: