Alicho sema Marjaiyya: Hakika kupitisha kanuni nzuri za uchaguzi sio jambo la vyama pekeyake na litawafanya wananchi wawe na moyo wa uchaguzi.

Maoni katika picha
Marjaa Dini mkuu hivi karibuni amesisitiza zaidi ya mara moja umuhimu wa kupitisha kakuni nzuri za uchaguzi zitakazo wapa moyo wananchi kuingia kwenye uchaguzi, akabainisha kua kupitisha kanuni zisizokua nzuri hazita kubalika wala hazitakua na tija, akaonyesha umuhimu wa kuundwa kanuni mpya za uchaguzi zinazo kubalika na wananchi.

Aliyasema hayo katika khutuba ya swala ya Ijumaa mwezi (17 Rabiul-Awwal 1441h) sawa na (15 Novemba 2019m) iliyo swaliwa ndani ya haram ya Imamu Hussein (a.s), chini ya Uimamu wa Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, lifuatalo ni tamko kuhusu swala hilo:

(Hakika uhalali wa serikali unategemea wananchi, hakuna anaye ipa haki kisheria zaidi ya mwananchi, matakwa ya raia huonekana kupitia matokeo ya uchaguzi huru na wa haki, hakika ni muhimu kutengeneza haraka kanuni za uchaguzi huru na wa haki utakao rudisha uwaminifu kwa wananchi bila kuwepo kwa upendeleo wa vikundi fulani au vyama vya kisiasa, itolewe nafasi ya mabadiliko ya kweli yatakayo onyesha tofauti kati ya serikali hiyo mpya na zilizo pita, kama wananchi watapenda kubadilisha viongozi wapya, kupitia uchaguzi huru na wa haki utakao kubaliwa na raia).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: