Msaada wa kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji upo kila mahala.

Maoni katika picha
Kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji (Liwaa/26 Hashdi Shaábi) kinaendelea na mradi wa kibinaadamu unaolenga kusaidia familia za mashahidi wa Hashdi Shaábi, uitwao (Hamlatul-Wafaa Al-Insaniyya), hivi karibuni mradi huo umetekelezwa katika mji mkuu wa Bagdad chini ya mkakati wa (kujitegemea) kwa wanafamilia wa mashahidi.

Mradi huu unalenga kuwasiliana na familia za mashahidi na kuwasaidia mambo ya aina mbalimbali hata kwa kiwango kidogo, ili familia hiyo iendelee kutegemea kitu hicho na kuifanya ijitegemee kuendesha maisha yake na kuwa na uhakika wa chakula katika maisha yao.

Chini ya utaratibu huo, muwakilishi wa kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji katika mji wa Diwaniyya, amekarabati nyumba ya Shahidi Qassim Khalf Matuki.

Jambo hili ni sehemu ya kuonyesha shukrani kwa familia zilizo jitolea watoto wao na wapenzi wao kwa ajili ya taifa, heshima na maeneo matakatifu.

Uongozi wa kikosi umesisitiza kuendelea kua karibu na familia za mashahidi na kusikiliza mahitaji yao pamoja na kuwapa misaada kwa ajili ya kuwapunguzia machungu na ugumu wa maisha.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: