Wananchi hawana chaguo zaidi ya kuendeleza madai yao kwa njia ya amani: yalisemwa na Marjaa Dini mkuu kwenye khutuba ya Ijuma (27/07/2018m).

Maoni katika picha
Wananchi hawana chaguo zaidi ya kuendeleza madai yao kwa njia ya amani, na kuonyesha matakwa yao kwa viongozi, wakisaidiwa na kila mtu mwenye uzalendo na taifa…, haya ndio aliyosema Marjaa Dini mkuu kuliambia bunge la sasa katika siku zake za kwanza, kufuatia maandamano ya wananchi yaliyofanywa wakati huo.

Aliyasema hayo katika khutuba ya pili ya swala ya Ijumaa mwezi (13 Dhul-Qaádah 1439h) sawa na (27 Julai 2018m), iliyo swaliwa ndani ya haram ya Imamu Hussein (a.s) chini ya uimamu wa Mheshimiwa Shekh Abdulmahdi Karbalai, lifuatalo ni tamko kuhusu swala hilo:

(bunge lijalo linatakiwa kuchukua hatua za kurekebisha mambo na kupitisha kanuni zitakazo wawezesha kufanya hivyo, kama serikali isipofanya mambo inayo ahidi au bunge lisipo tekeleza wajibu wake au idara ya mahakama wananchi watakua wahana budi zaidi ya kuendeleza madai yao kwa njia ya amani, kwa ajili ya kuonyesha matakwa yao kwa viongozi wakisaidiwa na kila mtu mwenye uzalendo na taifa, hapo hali itakua tofauti na leo, tunaomba tusifikie huko, akili itumike na kuweka mbele maslahi ya taifa, hasa kwa wale wenye mamlaka na maamuzi, wanatakiwa kuchukua hatua kabla mambo hayaja haribika, na Mwenyezi Mungu anawaongoza katika mafanikio).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: