Wito wa mavuno makubwa na kuongeza uchumi wa taifa kupitia kilimo.

Maoni katika picha
Shirika la teknolojia ya kilimo cha kisasa na viwanda Aljuud limetangaza kuanza kwa msimu wa kuandaa mashamba kwa kuzindua mbolea maalum ya kilimo cha ngano, ambayo inauwezo wa kuondoa chumvichumvi katika ardhi na inaongeza upambaji wa ngano kwa kiwango kikubwa, limetoa wito kwa wakulima wote walio weka oda ya mbolea wafike ofisi za shirika kwa ajili ya kupokea mbelea zao, na kuhakikisha msimu huu unakua na mavuno bora kulingana na mahitaji.

Shirika limewaomba wakulima wote wa ngano watumie mbolea hiyo katika msimu huu, kwani inauwezo mkubwa wa kuongeza kiwango cha uzalishaji wa ngano, mafanikio yake yameonekana mwaka jana, dunam moja ya ngano ilitoa kilo elfu mbili (tani 2) ambacho ni kiwango cha juu kabisa hapa Iraq, ukizingatia kua Atabatu Abbasiyya imeweka punguzo la bei, mbolea hizo zinapatikana kwa mawakala wa shirika waliopo sehemu mbalimbali nchini.

Kumbuka kua shirika la Aljuud lilianza kazi mwaka (2014m) kwa kutengeneza mbolea na bidhaa zingine za kilimo, mbolea hizi zinatengenezwa na kitengo maalum cha utafiti na uzalishaji, wakafanikiwa pia kutengeneza visafishio vya nyumbani na viwandani, wakapata maendeleo makubwa ndani ya muda mfupi hadi wakafikia kiwango cha juu cha uzalishaji.

Kuangalia bidhaa zinazo tengenezwa na shirika hili unaweza kutembelea vituo vya mauzo vya shirika vilivyopo ndani na nje ya Karbala, kwa maelezo zaidi piga simu namba (07801930125) au (07801035422), au fika kwenye kituo cha mauzo mubashara cha shirika kilichopo barabara ya (Karbala/ Najafu) mkabala na nguzo namba (1145).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: