Maahadi ya Quráni/ tawi la Najafu yahitimisha semina ya kufundisha matamsi ya herufi.

Maoni katika picha
Miongoni mwa semina zinazo lenga kufundisha matamshi sahihi ya herufi za kiarabu na usomaji wa kitabu cha Mwenyezi Mungu, idara ya usomaji katika Maahadi ya Quráni tukufu tawi la Najafu chini ya Atabatu Abbasiyya imehitimisha semina iliyo pewa jina la matamshi ya herufi (Makhaarijul-Khuruuf).

Mkufunzi wa semina hiyo alikua ni Dokta Karim Jibr Azzubaidi, amefundisha mada zaidi ya ishirini, ndani ya muda wa miezi mitatu, ametoa ufafanuzi wa kina kuhusu matamshi ya herufi za kiarabu, pia waliangalia tofauti kati ya rai za wachuchuoni wa zamani na wasasa chini ya ushiriki wa kundi kubwa la wadau wa Quráni, semina imefungwa kwa kuwatahini wanasema.

Fahamu kua hii ni semina ya mwisho katika mwaka wa 2019m, malengo makuu ya semina hizi ni kuhakikisha watu wanasoma Quráni tukufu kwa ufasaha.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: