Milango iliyo tengenezwa kwa weledi mkubwa wa fani za kiislamu.

Maoni katika picha
Ni milango iliyo tengenezwa kwa weledi mkubwa wa fani za kiislamu, kuanzia mpangilio wa mapambo, nakshi na rangi, hauwezi kuangalia milango hiyo bila kuvutiwa na mapambo pamoja na nakshi zake, hiyo ndio hali ya zaairu anapo wasili kwenye malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), huanza kukutana na milango yake ambayo humvutia kutokana na umaridadi wa mafundi walio tengeneza milango hiyo, iliyopambwa kwa maandishi mazuri na nakshi.

Atabatu Abbasiyya tukufu inamilango tisha, ambayo ni (mlango wa Kibla, mlango wa Imamu Hussan, mlango wa Imamu Hussein, mlango wa Imamu Swahibu Zamaan, mlango wa Imamu Kaadhim, mlango wa Imamu Jawaad, mlango wa Imamu Haadi (a.s), mlango wa Furaat –babu wa Algamiy-, mlango wa Imamu Ali (a.s) –baabu Kaf-), milango yote imewekwa kashi Karbalai baada ya upanuzi wa haram tukufu, milango hiyo imepambwa na aya za Quráni pamoja na nakshi za kiislamu na mapambo ya mimea yanayo endana na utukufu wa eneo hilo. Milango iliyopo hivi sasa ni matunda ya upanuzi wa Atabatu Abbasiyya tukufu, imepanuliwa na kuifanya iweze kuingiza idadi kubwa zaidi ya mazuwaru kwa urahisi, sambamba na kupanuliwa sehemu za kufanyia ibada za swala ziara na dua.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: