Watumishi wa Alkafeel wanaendelea kujenga paa la juu na taji la dirisha la malalo ya bibi Zainabu (a.s).

Maoni katika picha
Mafundi na wataalamu wa kiwanda cha Saqaa kinacho husika na utengenezaji wa madirisha na milango ya kwenye makaburi na mazaru tukufu chini ya Atabatu Abbasiyya, wanaendelea na kazi ya kutengeneza paa na taji la dirisha la kaburi la bibi Zainabu (a.s), kazi ambayo imepiga hatua kubwa, watakamilisha kazi hiyo baada ya muda mfupi, na kuingizwa katika orodha ya kazi zilizo tengenezwa na kiwanda hicho kwa mafanikio chini ya wananchi wazalendo wa Iraq na watumishi wa watu wa nyumba ya Mtume (s.a.w.w), kazi hii inafanywa baada ya makubaliano kati ya Atabatu Abbasiyya tukufu na mmoja wa watumishi wa Ahlulbait (a.s).

Tumeongea na Ustadh Husaam Muhammad Jawaad kuhusu utendaji wa kazi hiyo, ambaye ni makamo rais wa kitengo cha kutengeneza madirisha na milango ya kwenye makaburi, amesema: “Mwanzo wa kila kazi huwa kunahatua za awali, kuhusu hatua hizo sisi tuna wachoraji na wapambaji mahiri sana ambao ni raia wa Iraq, walipendekeza michoro kadhaa, tukaiwasilisha kwenye kamati maalum”. Akasema: “Baada ya kupasisha mchoro mmoja wa kazi hii ndipo kazi ikaanza mara maja”.

Akasisitiza kua: “Sasa hivi tupo katika hatua za mwisho, siku chache zijazo tutalipeleka Sirya na kuliweka juu ya dirisha takatifu”.

Akabainisha kua: “Sifa za dirisha hili ni:

  • 1- Lina urefu wa (mt4.3) na upana wa (mt3.sm11) kimo chake ni (mt2.75).
  • 2- Yametumika madini tofauti, yakiwemo chuma imara (chuma cha pua), fedha pamoja na mbao za Burimi ambazo zimetumika kutengeneza umbo la mbao lenye nakshi na mapambo, na dhahabu inayo kadiriwa kua (kg2).
  • 3- Nakshi zilizo tumika ni za mimea.
  • 4- Nakshi hizo zimebuniwa na kuchorwa na watalamu wenye weledi mkubwa.
  • 5- Umbo la mbao halionekani bayana, sehemu ya mbao na zingine zinamuonekano mmoja”.

Kumbuka kua mafundi wa Atabatu Abbasiyya wanaofanya kazi katika kiwanda cha kutengeneza madirisha na milango ya kwenye makaburi na mazaru tukufu, wana ujuzi na uzowefu mkubwa katika kazi hiyo, uwezo wao ulionekana wazi pale walipo tengeneza dirisha la kwenye kaburi la Abulfadhil Abbasi (a.s), ndio dirisha la kwanza kusanifiwa na kutengenezwa na raia wa Iraq, halafu wakatengeneza dirisha la Qassim (a.s) na milango ya malalo ya Sayyid Muhammad –Sabú-Dujail- na madirisha ya Maqaam ya Swafi-Swafa, bila kusahau dirisha la malalo ya Shekh Mufidi na Shekh Tusi pamoja na sehemu ya juu ya dirisha la Maimamu wawili Aljawadaini (a.s) na kazi zingine nyingi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: