Maahadi ya Quráni tukufu tawi la wanawake imehitimisha mfululizo wa semina za hukuzu za usomaji wa Quráni.

Maoni katika picha
Maahadi ya Quráni tukufu tawi la wanawake la mjini Bagdad chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imehitimisha semina tatu za hukumu za usomaji wa Quráni, idadi kubwa ya wasomaji wa Quráni imeshiriki katika semina hizo, kwa ajili ya kuboresha usomaji wao.

Kwa mujibu wa wasimamizi wa semina hizo, ni moja ya harakati zinazo fanywa na Maahadi katika sekta ya Quráni tukufu, Maahadi inazipa umuhimu mkubwa kutokana na faida inayo patikana kwenye semina hizo, ya kutengeneza kizazi cha wasichana wanaosoma Quráni kwa ufasaha mkubwa.

Wakaongeza kua: Semina hizo zimefanyika katika maeneo matatu ndani ya mji wa Bagdad, semina ya kwanza ilipewa jina la (Ahbaabu Hussein –a.s-), ya pili: (Almurtadhwa –a.s-), ya tatu: (Muhammad Mustwafa –s.a.w.w-), wakufunzi wa semina hizo wanauzowefu mkubwa katika sekta hiyo, wamefundisha kwa nadhariyya na vitendo.

Katika hafla ya kufunga semina hizo kimeshuhudiwa kisomo kizuri cha Quráni tukufu, pazia la usomaji huo wa Quráni lilifunguliwa na mwanafunzi Mahaasin Swahibu, kisha wakafuatia wanafunzi wengine, kila mwanafunzi aliye hifadhi Quráni alisoma ukurasa mmoja kwa kuanzia surat Fat-hu hadi mwisho wa msahafu, baada ya hapo ukasomwa wimbo wa Atabatu Abbasiyya tukufu (Lahnul-Ibaa) na kundi la wanafunzi, kundi lingine la wanafunzi likasoma mifano ya hukumu za nuni sakina na tanwini.

Kutokana na juhudi zilizo onyeshwa na wanafunzi pamoja na walimu wao, wanasemina wametunukiwa vyeti, na hafla ikafungwa kwa kusoma Duaau Faraj ya Imamu Mahdi (a.f).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: