Toleo jipya katika kituo cha turathi za Hilla: (Makala ya picha za muhtasari wa maneno katika kuwatambua watu).

Maoni katika picha
Kituo cha turathi za Hilla chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kinaendelea na harakati za uandishi, uhakiki na utafiti katika sekta ya turathi na nafasi ya nakala kale, kisha kuchapisha kwa muonekano unao endana na utukufu wake na kuvifanya kua tayali kwa kutumiwa na watafiti pamoja na wanafunzi.

Hivi karibuni (Kimechapisha Makala za picha za muhtasari wa maneno ya kuwatambua watu), nacho ni kitabu cha nakala mbili, ya kwanza: ni nakala iliyopo katika hazina ya Ayatullah Sayyid Hassan Swadri (q.s) ya mwaka (715h) iliyo kua inasomwa na Allamah. Pili: Nakala iliyo andikwa na Ali bun Muhammad Twabari mwaka wa (744h) katika Mash-hadi Alawiy takatifu, nakala mbili zimewekwa pamoja na kutoa kitabu cha (muhtasari wa maneno) katika umbo linalo kalibiana na matakwa ya muandishi (r.a) na kwa ajili ya kupata faida.

Mtafiti bwana Maitham Sawidani Alhamiri ameandika utangulizi mzuri ulio bainisha tofauti zilizopo baina ya nakala hizo, ambazo zimechapishwa chini ya usimamizi wa kituo cha turathi za Hilla chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu.

Kwa kuangalia kitabu hicho pamoja na vitabu vingine, tembelea maonyesho ya vitabu yaliyopo karibu na mlango wa Kibla wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: