Kwa mujibu wa maelezo ya wasimamizi wa shughuli hiyo, huduma walizo pewa zinahusisha ugawaji wa chakula, milo yote mitatu kila siku, sambamba na kua pamoja nao katika maandamano kila siku hadi madai yao kisheria yatakapo fanyiwa kazi.
Kumbuka kua idara ya ustawi wa jamii imekua mstari wa mbele kusaidia waandamanaji tangu siku ya kwanza ya maandamano haya katika uwanja wa uhuru (tahriiri) mjini Bagdad, na baadae katika viwanja vyote vya waandamanaji kwenye mikoa mingine, miongoni mwa huduma zinazo tolewa ni:
- - Kujenga vibanda vya kutolea huduma.
- - Kupika chakula na kukigawa kwa waandamanaji.
- - Kugawa maji na juisi.
- - Kutoa huduma za matibabu.
- - Kutoa huduma ya uokozi kwa wahanga wa maandamano.
- - Kutoa msaada wa kimaana kwa kuwepo idadi kubwa ya watumishi kwenye uwanja wa maandamano.
- - Kutoa baadhi ya vifaa vinavyo tumiwa na waandamanaji.
- - Kusaidia kufanya usafi katika maeneo yanayo tumiwa na waandamanaji.