Katika khutuba ya pili ya swala ya Ijumaa iliyo swaliwa ndani ya haram tukufu ya Imamu Hussein (a.s) leo (30 Rabiul-Awwal 1441h) sawa na (27 Desemba 2019m) chini ya uimamu wa Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, ameongelea nukta nyingi kuhusu mazingira tunayo ishi kwa sasa, miongoni mwa aliyo sema ni:
- - Katika kila sekta ya maisha yetu, tunatakiwa kupata ushauri wa wenye akili na hekima na kupuuza ushauri wao husababisha majuto.
- - Haifai kufikiri kua unajua kila kitu wakati kuna wajuzi zaidi yako na wenye akili na hekima kukushinda.
- - Tukitaka kufanikiwa katika maisha yetu kisiasa, kiuchumi na kijamii, yatupasa kuwa na maamuzi salama, ili kufanya maamuzi salama inahitaji maono.
- - Watu wenye akili na hekima hawana ushauri mbaya wala hawafanyi mambo kwa jazba.
- - Watu wenye akili na hekima huangalia jambo pande zote na hufanya maamuzi salama.
- - Baadhi ya wakati mwanaadamu anahitaji mnasihi na mshauri.
- - Kuna watu wanauwezo wa kubaini tatizo na kulitatua.
- - Kuwepo watu wenye akili na hekima kwenye kila jamii ni neema.
- - Mwanaadamu anahitaji watu wenye akili na ushauri kwa ajili ya kumshauri ili aweze kujinasua kwenye matatizo.
- - Tatizo sio la mtu mwenye akili na hekima bali kwa yule asiye sikiliza ushauri wao.
- - Tatizo sio la mtu mwenye akili na hekima bali tatizo kwa mtu anayejiona kua ana akili na hekima wakati hana.
- - Ninapo jua kua naumwa natakiwa kwenda kwa daktari na kufuata maelekezo yake.
- - Kila mtu anahitaji ushauri wa watu wingine mwenye uwezo maarifa na uzowefu.
- - Mwenye elimu, akili na hekima anaweza kufanya maamuzi salama.
- - Katika kuitendea haki nafsi unatakiwa kusikiliza ushauri wa watu.
- - Kama tunavyo chagua chakula kizuri pia tunatakiwa tuchague fikra nzuri na kufanyia kazi ushauri wa wenye akili na hekima.
- - Mwanaadamu anatakiwa kufahamu sura yake halisi baadhi ya vioo huonyesha sura tofauti na ulivyo, hali iko hivyo katika kuamiliana na watu baadhi ya ushauri huwa sio mzuri yapasa kuwafuata wenye akili na hekima.
- - Kila mtu anahitaji kupata ushauri na muongozo wa namna ya kujinasua katika matatizo aliyo nayo.
- - Mtu mwenye akili ni yule anayetafuta utatuzi wa matatizo na kuufanyia kazi.