Kwa mujibu wa maelezo ya kitengo cha usimamizi wa haram, vizuwizi hivyo vinatumika kupangilia matembezi ya mazuwaru na kuondosha msongamano, hususan kwenye ziara zinazo hudhuriwa na mamilioni ya watu pamoja na siku za Ijumaa, pia vinatenganisha baina ya wanaume na wanawake, wakati wa swala za jamaa, na vinatumika kubeba vitabu vya dua, ziara pamoja na misahafu, na kuhifadhi turba, kwa sababu vina tabaka tatu, miongoni mwa sifa kubwa za vizuwizi hivyo ni:
- - Vizuwizi vipo themanini (80) vimetengenezwa kwa weledi mkubwa na kuwekwa nakshi na mapambo ya Atabatu Abbasiyya tukufu.
- - Kila kizuwizi kina urefu wa mita moja na upana wa mita mbili, kina sehemu tatu, sehemu ya juu inavitabu vya dua na ziara pamoja na misahahu, na sehemu mbili za chini kuna turba na vitu vingine.
- - Vina rangi nzuri na ubora wa hali ya juu.
- - Vina hamishika kwa urahisi.
- - Vinapangika kwa urahisi.
- - Vyote vinaukubwa sawa.
- - Vinatumia nafasi ndogo ndani ya haram tukufu tofauti na vizuwizi vya zamani.
Fahamu kua vipimo vya vizuwizi hivi viliandaliwa na kutengenezwa na jopo la wahandisi na mafundi wa Atabatu Abbasiyya tukufu, kisha kukabidhiwa kwenye kitengo cha usimamizi wa haram, halafu vikaunganishwa na kitengo cha usimamizi wa haram na kuwekwa sehemu mbalimbali ndani ya haram.