Yalisemwa na Marjaa Dini mkuu: watu wa nje kuingilia mambo ya ndani ni hatari na mwenye hasara kubwa ni raia wa Iraq

Maoni katika picha
Marjaa Dini mkuu ametahadharisha mara nyingi madhara ya watu wa nje kuingilia mambo ya kitaifa, ni hatari ambayo hupelekea nchi kua uwanja wa vita ya kitaifa na kimataifa, akasema kua jambo hilo la (uingiliaji wa watu wa nje halikubaliki).

Alirudia kusisitiza jambo hilo katika khutuba ya mwezi (17 Rabiul-Awwal 1441h) sawa na (15/11/2019m) iliyo tolewa na Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi ndani ya haram ya Imamu Hussein (a.s), lifuatalo ni tamko kuhusu swala hilo:

(Hakika vita ya islahi wanayo pigana wananchi wa Iraq ni vita ya kizalendo inayo husu wananchi wa Iraq peke yake, wao ndio wanaopaswa kupigana vita hiyo, haifai kuruhusu kusaidiwa na watu wa nje kwa aina yeyote ile, kusaidiwa na watu wa nje ni hatari na kunaweza kulifanya taifa kua uwanja wa vita na sehemu ya kutekeleza agenda za watu wengine na mwenye hasara kubwa atakua na raia wa Iraq).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: