Atabatu Abbasiyya tukufu imepambwa kuadhimisha kuzaliwa kwa bibi Zainabu (a.s).

Maoni katika picha
Mazingira wa furaha yametanda katika Atabatu Abbasiyya tukufu kufuatia kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Aqilatu-Twalibina bibi Zainabu (a.s), korido za Ataba tukufu zimepambwa vizuri kufuatia kumbukumbu hiyo tukufu, vitambaa vilivyo andikwa maneno ya kumtukuza vimewekwa kwenye kuta za Ataba kutokana na utukufu alionao bibi huyo ndani ya nyoyo za wafuasi wa Ahlulbait (a.s).

Kama kawaida Atabatu Abbasiyya tukufu imeandaa ratiba maalum ya kuadhimisha tukio hilo, miongoni mwa vipengele muhimu kwenye ratiba hiyo ni kufanya hafla ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), itakayo husisha usomaji wa mashairi yatakayo elezea utukufu wa bibi Zainabu (a.s) pamoja na mambo mengine.

Kumbuka kua wafuasi wa Ahlulbait (a.s) kila sehemu ya dunia huadhimisha tukio hili tukufu, sambamba na maadhimisho ambayo hufanywa katika malalo yake takatifu mjini Damaskas Sirya mwezi tano Jamadal-Uula, ambayo inasadifu siku aliyo zaliwa Aqilatu-Twalibina, Thauratul-Haqu, mnara wa waongofu bibi Zainabu Al-Akbar mtoto wa kiongozi wa waumini (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: