Uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu umepambwa kwa miti na maua ya kusherehekea kumbukumbu ya kuzaliwa kwa bibi Zainabu (a.s), ambaye mazazi yake yanasadifu Jumatano ya kesho, maua yamewekwa kwenye uwanja wa katikati ya haram mbili na katika maeneo yaliyo pauliwa pamoja na sehemu zinazo zunguka haram ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), kwa namna ambayo inatia furaha na kuonyesha ukubwa wa tukio hilo.
Kikosi cha shamba boy wa Alkafeel kama kawaida yao kwenye kila tukio, kimechukua jukumu la kuweka mapambo hayo, kimeweka miti na maua sambamba na kutengeneza mapambo mengine mazuri.
Yamefanywa yote hayo kutokana na utukufu wa maadhimisho haya kwa waislamu wanaokuja kumpongeza Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) kufuatia tukio hili adhim.
Haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) imewekwa mabango na taa za rangi kwenye milango yake, hali kadhalika imepambwa na bendera za kijani zilizo andikwa ujumbe maalum kuhusu maadhimisho haya, kama sehemu ya ratiba maalum ya Atabatu Abbasiyya tukufu katika kuadhimisha kuzaliwa kwa Aqilatu-Hashimiyyin.