Miongoni mwa harakati za Skaut hatua ya kwanza, Jumuiyya ya Skaut ya Alkafeel katika Atabatu Abbasiyya tukufu imetoa mafunzo mbalimbali kwa wanachama wake, wameshiriki zaidi ya wanachama sitini, mafunzo ya kwanza yalipewa jina la (uratibu na uchungaji wa muda), wamefundishwa kua; kitu muhimu katika mafanikio ya mwanaadamu ni namna ya kutumia muda, wamefundishwa kwa kutumia njia za kisasa na wakapewa mazowezi yanayo endana na upeo wa fikra za vijana.
Jambo la pili wamefundishwa: (mbinu za mafanikio na kujitegemea), wakufunzi wameongea kuhusu misingi ya mafanikio, na namna ya kujiamini na kufanikisha malengo binafsi, jambo la tatu wakafundishwa mambo ya kiimani kwa kikosi cha Jawaalah.
Katika kujenga uzalendo wa wanaskauti, wamefundishwa mambo ya kitaifa pamoja na baadhi ya maelekezo ya Marjaa Dini mkuu.
Kumbuka kua program ya mafunzo ya Skaut hatua ya kwanza ilianza siku za nyuma na imechukua wiki nane (8), walikua wanafundishwa siku ya Ijumaa na Jumamosi kila wiki.