Yalisemwa na Marjaa Dini mkuu miezi miwili iliyo pita katika khutuba ya Ijumaa (3 Rabiul-Awwal 1441h) sawa na (1 Novemba 2019m), iliyo swaliwa ndani ya haram ya Imamu Hussein (a.s), chini ya uimamu wa Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, alisema kua wananchi wa Iraq peke yao ndio wenye haki ya kupambana katika vita ya islahi, haifai kwa mtu yeyote au kikundi chochote kutoka ndani au nje ya nchi kuwaamulia wairaq mambo yao.
Lifuatalo ni tamko kuhusu swala hilo:
Kuheshimu matakwa ya raia wa Iraq katika kuchagua mfumo wa siasa na utawala wa taifa lao, kwa kupiga kura ya maoni ya katiba na kufanya uchaguzi wa bunge, ni jambo linalo tiliwa manani na Marjaa Dini mkuu, amekua akisisitiza jambo hilo tangu kuanguka kwa utawala uliopita, leo anasisitiza kua japokua islahi ni jambo la lazima –kama lilivyo zungumzwa mara nyingi- jambo la kuzingatiwa ni kwamba vita ya islahi inapaswa kufanywa na wananchi wa Iraq wa tabaka zote, haitakiwi mtu yeyote au kikundi chenye mlengo fulani kuwaamlia wananchi wa Iraq kwa kuangalia maslahi yake.
Tunawaomba watu wote waweke mbele mustakbali wa taifa, wasiangalie maslahi binafsi na kushindwa kufanya maamuzi sahihi katika swala hili, yenye faida kwa taifa (na Mwenyezi Mungu huongoa katika wema naye ni mkuu wa kufanikisha).