Baina ya haram za ndugu wawili: yafanywa hafla ya kuadhimisha mazazi ya bibi Zainabu (a.s).

Maoni katika picha
Katika mazingira yaliyojaa furaha jirani na haram ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), imefanywa hafla ya kuadhimisha na kukumbuka kuzaliwa kwa bibi Zainabu (a.s) pamoja na kongamano la usomaji wa mashairi ambalo wameshiriki washairi mbalimbali.

Kongamano hilo limehudhuriwa na idadi kubwa ya mazuwaru, washairi na waimbaji wa kaswida wamepamba shughuli hiyo kwa mashairi na kaswida nzuri kuhusu maadhimisho hayo.

Wamesoma mashairi na kaswida zilizo onyesha mapenzi kwa Ahlulbait (a.s), na umuhimu wa kufuata mwenendo wao na kushikamana na mafundisho yao sambamba na kuhuisha utajo wao, pamoja na kuingiza furaha katika moyo wa Imamu wa zama (a.f).

Fahamu kua kongamano hili hufanywa kila mwaka chini ya usimamizi wa kitengo kinacho simamia eneo la katikati ya haram mbili tukufu, kawaida ya kitengo hiki huomboleza na kuadhimisha tarehe za kuzaliwa au kufariki kwa Imamu Maasumu (a.s) na maswahaba wa karibu (r.a).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: