Kufuatia kumbukumbu ya kuzaliwa kwa bibi Zainabu (a.s): majina ya washindi wa shindano la kisa kifupi kuhusu bibi Zainabu na dua ya Tawassul yatangazwa.

Maoni katika picha
Kufuatia kumbukumbu ya kuzaliwa kwa bibi Zainabu (a.s), kituo cha utamaduni wa familia chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, kimetangaza majina ya washindi wa shindano la kisa kifupi kuhusu bibi Zainabu linalo itwa: (shindano la kisa cha Zainabiyya), pamoja na washindi wa shindano la dua tawassul na kuwapa zawadi.

Yamefanywa hayo katika hafla iliyo fanywa na kituo hicho, washindi watano wamepewa zawadi, nao ni:

  • - Suzan Abdallah/ kutoka Najafu, kisa chake kinaitwa (kukutana katika yakini).
  • - Zaharaa Hussam Shaharibali/ kutoka Najafu, kisa chake kinaitwa (Jua na mwezi huenda kwa hisabu).
  • - Hamida Qassim/ kutoka Basra, kisa chake kinaitwa (upanga wa kubainisha).
  • - Narjisi Swafi/ kutoka Baabil, kisa chake kinasema (bila jabali hakuna muinuko)
  • - Zainabu Dhiyaai/ kutoka Najafu, kisa chake kinaitwa (kiburi cha jabali).

Vikafuata vipengele vingine vya hafla ikiwa ni pamoja na kutangazwa washindi wa shindano la dua tawassul lililo isha siku chache zilizo pita, hafla hiyo imehudhuriwa na viongozi wa vikundi vya wakina mama kutoka ndani na nje ya Atabatu Abbasiyya.

Fahamu kua shindano la kisa cha Zainabiyya linalenga kuangazia nafasi ya bibi Zainabu (a.s) katika kunusuru harakati ya Imamu Hussein (a.s), mada zilizo shindaniwa zilikua ni:

  • 1- Nafasi ya habari kuhusu bibi Zainabu (a.s).
  • 2- Subira ya bibi Zainabu (a.s).
  • 3- Msimamo wa bibi Zainabu (a.s).
  • 4- Ufasaha wa bibi Zainabu (a.s).
  • 5- Kulelewa kwa bibi Zainabu (a.s) na uhusiano wake kifamilia na kijamii.

Kumbuka kua kituo cha utamaduni wa familia kimejikita matika mambo yanayo husu familia na jamii, ofisi zake zipo Karbala/ mtaa wa Mulhaq/ barabara ya hospitali ya Hussein (a.s) katika jengo la kituo cha Swidiiqah Twahirah (a.s). kwa maelezo zaidi piga simu ifuatayo: (07828884555).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: