Malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) imefurika mazuwaru… ziara ya pongezi.

Maoni katika picha
Malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) baada ya Adhuhuri ya Alkhamisi (6 Jamadal-Uula 1441h) sawa na (2 Januari 2020m) imeshuhudia idadi kubwa ya mazuwaru, jambo hilo limezoweleka kila ufikapo usiku wa Ijumaa.

Lakini Ijumaa hii tofauti na zingine, kwani imesadifu kumbukumbu ya mtukufu na kipenzi mkubwa kwa kila zaairu, kumbukumbu ya kuzaliwa kwa dada yake bibi Zainabu (a.s), ambaye alizaliwa tarehe kama ya jana, hivyo watu wengi wamekuja kumzuru Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa ajili ya kumpongeza na kuonyesha furaha kwa jambo hilo, utaona pia mazuwaru wanapongezana wakati wakielekea kwenye kaburi takatifu kutoa pongezi.

Kama kawaida ya Atabatu Abbasiyya kila siku ya Ijumaa, imejiandaa vyema kuhudumia mazuwaru walio furika ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na maeneo yanayo zunguka haram.

Kamera ya mtandao wa Alkafeel inakuletea baadhi ya picha za mazuwaru hao wakati wakimiminika kuingia katika malalo tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: