Muhimu na hivi punde.. nakala kamili ya khutuba ya Ijumaa: taifa linaelekea katika wakati mgumu tunaomba uvumilivu.

Maoni katika picha
Mwakilishi wa Marjaa Dini mkuu Mheshimiwa Shekh Abdulmahadi Karbalai katika khutuba ya Ijumaa ya leo (7 Jamadal-Uula 1441h) sawa na (3 Januari 2020m) iliyo swaliwa ndani ya haram ya Imamu Hussein (a.s), amesoma nakala kutoka ofisi ya Marjaa Dini mkuu katika mji wa Najafu.

Mheshimiwa Shekh Abdulmahdi Karbalai amesema: Mabwana na mabibi.. tunakusomeeni nakala iliyo tufikia kutoka ofisi ya Mheshimiwa Ayatullah Sayyid Sistani isemayo:

Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema mwenye kurehemu

Mambo yanaenda kwa kasi na taifa linapitia wakati mgumu, kuanzia tukio ka kushambuliwa wanajeshi wa Iraq katika mji wa Qaaim, lililo pelekea kufa kishahidi makumi ya wanajeshi wetu, hadi matukio ya kusikitisha yaliyo tokea Bagdad siku za hivi karibuni, na shambulizi la kinyama karibu na uwanja wa ndege wa Bagdad usiku uliopita linalo vunja heshima ya Iraq na mikataba ya kimataifa, shamulio ambalo limepoteza maisha ya idadi kubwa ya majemedari wa vita dhidi ya magaidi wa Daesh.

Hakika matukio haya na mengine yanaashiria kua taifa linaelekea katika wakati mgumu sana, tunawaomba wenye mamlaka kuwa na subira na kufanya maamuzi kwa hekima, tunainua mikono kumumba Mwenyezi Mungu mkuu alilinde taifa la Iraq na raia wake kutokana na kila aina ya shari na njama za maadui.

Ewe Mola nyoyo zetu tunazielekeza kwako, na shingo zetu tumeinua kwake, macho yanaangalia kwako na miili yetu inakunyenyekea wewe, ewe Mola hazina za shari zimefunguka, ewe Mola tunakushtakia kuharibika kwa hali zetu, na wingi wa maadui zetu, na uchache wa idadi yetu, tupe faraja kutoka kwako ewe Mola, na nusra yako, kwa rehema yako ewe mwingi wa rehema, Aamina Rabbal-Aalamina.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: