Marjaa Dini mkuu: kuuawa kishahidi kwa majemedari wa vita dhidi ya magaidi wa Daesh kunaashiria kua taifa linaelekea katika hali ngumu sana.

Maoni katika picha
Marjaa Dini mkuu amesema kua; kuuawa kishahidi kwa majemedari wa vita dhidi ya magaidi wa Daesh kunaashiria kua taifa linaelekea katika hali ngumu sana, akasema kua shambuzi hilo linavunja heshima ya Iraq na mikataba ya kimataifa.

Hayo yamesemwa kwenye khutuba ya swala ya Ijumaa leo mwezi (7 Jamadal-Uula 1441h) sawa na (03 Januari 2020m) ndani ya haram ya Imamu Hussein (a.s), iliyo tolewa na Mheshimiwa Shekh Abdulmahdi Karbalai, lifuatalo ni tamko kuhusu swala hilo:

(Matukio ya kusikitisha yaliyo tokea Bagdad siku za hivi karibuni, na shambulizi la kinyama karibu na uwanja wa ndege wa Bagdad usiku uliopita linalo vunja heshima ya Iraq na mikataba ya kimataifa, shamulio ambalo limepoteza maisha ya idadi kubwa ya majemedari wa vita dhidi ya magaidi wa Daesh. Hakika matukio haya na mengine yanaashiria kua taifa linaelekea katika wakati mgumu sana).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: