Baada ya matukio yanayo ashiria taifa la Iraq linaelekea katika wakati mgumu sana Marjaa Dini mkuu ametoa wito wa kufanya mambo wa hekima na kua wavumilivu.
Ameyasema hayo kwenye khutuba ya Ijumaa leo (7 Jamadal-Uula 1441h) sawa na (3 Januari 2020m) ndani ya haram ya Imamu Hussein (a.s) iliyo tolewa na Mheshimiwa Shekh Abdulmahdi Karbalai. Lifuatalo ni tamko kuhusu swala hilo:
(Tunawaomba wenye mamlaka kuwa wavumilivu na kufanya mambo kwa hekima, tunainua mikono kumumba Mwenyezi Mungu mkuu alilinde taifa la Iraq na raia wake kutokana na kila aina ya shari na njama za maadui).