Marjaa Dini mkuu ahitimisha khutuba yake kwa kusoma dua na amewaomba wanaoswali kufuatiliza kisomo chake.
(Ewe Mola roho zetu tunazielekeza kwako, na shingo zetu tumeinua kwako, macho yanaangalia kwako na miili yetu inakunyenyekea wewe, ewe Mola hazina za shari zimefunguka, ewe Mola tunakushtakia kuharibika kwa hali zetu, na wingi wa maadui zetu, na uchache wa idadi yetu, tupe faraja kutoka kwako ewe Mola, na nusra yako, kwa rehema yako ewe mwingi wa rehema, Aamina Rabbal-Aalamina).