Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya zimepokea msafara wa washindikizaji wa jeneza za waliopata shahada katika shambulizi la Mmarekani ambao ni majemedari wa Hashdi Shaábi.

Maoni katika picha
Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya baada ya Magharibi na Isha ya leo Jumamosi (8 Jamadal-Uula 1441h) sawa na (4 Januari 2020m), zimepokea misafara ya kushindikiza mashahidi wa Hashdi Shaábi walio itikia fatwa ya jihadi ya kujilinda takatifu na kushambuliwa na wamarekani karibu na uwanja wa ndege wa kimataifa Bagdad.

Mapokezi ya mashahidi hao yameongozwa na makatibu wakuu wa Ataba hizo pamoja na manaibu wao na wajumbe wa kamati kuu za Ataba zote mbili ikiwa ni pamoja na watumishi wa ataba hizo, aidha idadi kubwa ya wanajeshi na vongozi wameshiriki katika mapokezi hayo, bila kusahau idadi kubwa ya watu wa Karbala iliyo jitokeza sambamba na mazuwaru wa malalo mbili takatifu, misafara ya watu hao imeanzia barabara ya Kibla kuelekea katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) hadi kwenye malalo ya bwana wa mashahidi (a.s), na kupokelewa ndani ya haram ya Imamu Hussein na kiongozi mkuu wa kisheria wa Ataba hiyo Mheshimiwa Shekh Abdulmahdi Karbalai.

Baada ya kufanya ziara kwa niaba yao ndani ya malalo ya Imamu Hussein (a.s), wakapelekwa katika malalo ya mnyweshaji wenye kiu Karbala (a.s), wakapita kwenye uwanja wa katikati ya haram mbili, na wakapokelewa na kiongozi mkuu wa kisheria wa Atabatu Abbasiyya Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, halafu wakafanya ibada ya ziara kwa niaba ndani ya haram hiyo na kuwatakia rehema mashahidi watukufu, wakamuomba Mwenyezi Mungu awaingize katika rehema zake tukufu na awape subira wapenzi wao na familia zao hakika yeye ni mwingi wa kusikia na mwingi wa kujibu.

Kumbuka kua uongozi mkuu wa Ataba mbuli Husseiniyya na Abbasiyya ulitoa mkono wa pole na kutangaza msiba kupitia minara ya Ataba hizo takatifu Husseiniyya na Abbasiyya, wameswaliwa swala ya jeneza mara mbili, mara ya kwanza katika uwanja wa katikati ya haram mbili chini ya uimamu wa Shekh Abdulmahdi Karbalai, na mara ya pili ndani ya haram ya Abulfdhil Abbasi (a.s) chini ya uimamu wa Sayyid Swafi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: