Mbele ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s): maafisa wapya wakijeshi wamekula kiapo cha utii na kulitumikia taifa la Iraq.

Maoni katika picha
Katika tukio la kizalendo, maafisa wapya wa kijeshi waliohitimu masomo yao kwenye vyuo vya kijeshi hapa Iraq, wamefanya ziara katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na kula kiapo cha utii kwa pamoja mbele ya malalo hiyo takatifu, wameahidi kulitumikia taifa la Iraq na kulinda ardhi na raia wake bila ubaguzi.

Baada ya kula kiapo maafisa hao wameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Hakika kiapo hiki ni sawa na kuahidi kulitumikia taifa letu kwa ukamilifu, na kulinda amani ya Iraq dhidi ya magaidi na wahalifu, kwa sababu kiapo hiki kinatolewa mbele ya kiongozi mtukufu Abulfadhil Abbasi (a.s)”.

Maafisa hao wamepokelewa na watumishi wa idara ya utawala kitengo cha uhusiano katika Atabatu Abbasiyya tukufu, na wakaongozana nao katika ibada ya ziara.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: