Haifai kusahau utukufu wao.. idara ya ustawi wa jamii chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu: kusaidia wapiganaji waliopo katika uwanja wa vita ni kipaombele chetu.

Maoni katika picha
Idara ya ustawi wa jamii chini ya Atabatu Abbasiyya, kutoa misaada ya kibinaadam ndio kipaombele chake, kazi yetu inaendelea pamoja na mazingira tunayo pitia kama taifa, tunagawa vitu wanavyo hitaji wapiganaji kama vile chakula na vinginevyo, kwa kiasi ambacho inawawezesha kuendelea kupambana na kila mtu anayetaka kuharibu amani na utulivu wa taifa, kwa ufupi tunaweza kusema kua; misaada hii ni sehemu ya kufanyia kazi agizo la Marjaa Dini mkuu Mheshimiwa Sayyid Sistani katika moja ya matamko yake ya hivi karibuni alisema kua: (… Haifai kusahau utukufu wao…) kauli hiyo imetafsiriwa kwa vitendo na ofisi zetu zilizopo kwenye mikoa tofauti ya Iraq.

Huu hapa msafara wa Answaru Hussein (a.s) chini ya mawakibu za mkoa wa Bagdad, wanatekeleza jukumu lao na kutuma msafara wa kutoa misaada kwa wizara ya ulinzi, hadi kwa wapiganaji waliopo katika mji wa Buhairaat Iskandariyya mkoani Baabil, na kuwapa vitu mbalimbali, haya ndio yaliyo ambiwa mtandao wa Alkafeel na Abu Aiman Abudi kiongozi wa msafara wa Answaaru Hussein (a.s), akaongeza kua: “Tunaendelea kutoa misaada kila sehemu chini ya utaratibu maalum, baada ya kupokea maombi kutoka kwa wapiganaji hao, hufungwa safari na kupelekwa misaada inayo hitajika na wapiganaji hao ili kuwafanya waimarike zaidi katika kutekeleza jukumu lao”.

Misaada hiyo iliweza kuunganisha mji wa Tal-Afar, hivi karibuni idara ya ustawi wa jamii imefunga safari na kwenda katika vikosi mbalimbali vya wapiganaji, kikiwemo kikosi cha Liwaau/44 Hashdi Shaábi (Answaru Marjaiyya) kinacho linda amani katika mji wa Hadhar, wanaendelea kupigana na mabaki ya Daeshi kila baada ya muda, pamoja na Liwaau/25 Hashdi Shaábi wamepewa zawadi ya vitu tofauti walivyo kua wanahitaji.

Wapiganaji wameshukuru sana kazi zinazo fanywa na idara ya ustawi wa jamii ya Atabatu Abbasiyya ya kuwasaidia bila kuchoka.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: