Yalisemwa na Marjaa Dini mkuu: watu wenye hekima na akili huangalia mambo pande zote, na hufanya maazuzi maziri na salama.

Maoni katika picha
Marjaa Dini mkuu amesisitiza umuhimu wa kusikiliza ushauri wa watu wenye akili na hekima ili kufanya maamuzi sahihi na salama katika maisha, kwa sabababu watu wenye akili na hekima hawatoi ushauri mbaya wala hawaendeshwi na jazba, huangalia jambo kwa undani na hufanya maamuzi sahihi na salama.

Aliyasema hayo kwenye khutuba ya pili ya swala ya Ijumaa mwezi (30 Rabiul-Aakhar 1441h) sawa na (27 Desemba 2019m), iliyo swaliwa ndani ya haram ya Imamu Hussein (a.s) chini ya uimamu wa Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, lifuatalo ni tamko kuhusu swala hilo:

(Watu wenye akili na hekima hawatoi ushauri mbaya wala hawasukumwi na jazba, huliangalia jambo katika pande zote, na hufanya maamuzi mazuri na salama).

Akaongeza kua: (Watu wenye akili, maono na hekima ni neema katika kila jamii, mtu anatakiwa awafuate watu hao ili wamuelekeze namna ya kujinasua katika tatizo alilo nalo, ukiangalia katika historia mara nyingi mtu anayefuata ushauri wa watu wenye akili na hekima hadumbukii kwenye tatizo, bali asilimia kubwa ya watu wanaopata matatizo ni wale wanaopuuza ushauri wa wenye akili na hekima, tatizo lingine pia ni kwa watu wanaojiona wana akili na hekima, mtu kujiita kua anahekima na akili hakumfanyi awe navyo, mtu wa aina hiyo hawezi kufahamu mambo mengi kwa sababu ameizuwia nafsi yake kutafuta ukweli).

Akasema: (Nilisema kua tatizo halipo kwa watu wenye akili na hekima, bali tatizo lipo kwa watu wasio sikiliza ushauri au wanasikiliza lakini hawaufanyii kazi, kila mtu anapitia mazingira tofauti katika maisha yake, kuna wakati anahitaji kupata ushauri na maelekezo kuhusu namna ya kujinasua katika tatizo alilo nalo, mtu hufurahi anapopata ufumbuzi wa tatizo lake).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: