Maahadi ya Quráni tukufu tawi la wanawake imepata zawadi za ushindi katika shindano la usomaji wa Quráni na naghma la kitaifa

Maoni katika picha
Maahadi ya Quráni tukufu tawi la wanawake chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu imepata nafasi za juu katika shindano la nne kwa wanawake la kuhifadhi Quráni na usomaji wake, ambalo ni sehemu ya kujiandaa na shindano la kimataifa linalo andaliwa na kituo cha kitaifa cha maarifa ya Quráni chini ya uongozi wa wakfu Shia, kwa kushirikiana na Darul-Quráni ya Atabatu Husseiniyya tukufu.

Ustadhat Rim Muhammad Mahadi kutoka Maahadi ya Quráni tawi la wanawake mjini Bagdad amepata nafasi ya kwanza, na Ustadhat Hauraa Aamir Yasin kutoka tawi la Waasit akapata nafasi ya pili kwenye usomaji na naghma, sekta inayo lenga kutambua vipaji vya usomaji wa Quráni, aidha ndio shindano muhimu sana katika mashindano ya usomaji wa Quráni, baada yao wakafuata washiriki wengine ambao wamesha wahi kusoma katika vikao vya usomaji wa Quráni vya kimataifa, ambao jumla walikua (72) wakiwemo mahafidh (walio hifadhi Quráni) na wasomaji wa kawaida, shindano hili limefanyika kwa muda wa siku nne.

Kwa mujibu wa wasimamizi wa Maahadi ya Quráni tawi la wanawake katika Atabatu Abbasiyya kutufu wamesema kua: ushindi huu haujapatikana bure, ni matokeo ya juhudi kubwa inayo fanywa na msaada endelevu kutoka kwa viongozi wa kitengo na uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu, ambao wameiwezesha Maahadi ya Quráni tawi la wanawake kufanya vizuri kwa kuweka mazingira wezeshi kwa wanawake, ushindi huu ni ushahidi wa wazi wa kazi nzuri wanayofanywa.

Kumbuka kua hii sio mara ya kwanza ambayo wasomaji wa Quráni katika Maahadi kitengo cha wanawake wanapata ushindi, wameshiriki sehemu nyingi na kupata nafasi za juu, inaonyesha uzuri wa mfumo wa ufundishaji unaotumiwa na Maahadi pamoja na uzuri wa idara.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: