Atabatu Abbasiyya tukufu yapanga ratiba ya maombolezo katika kukumbuka kifo cha bibi Fatuma Zaharaa (a.s).

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu asubuhi ya Jumanne (11 Jamadal Uula 1441h) sawa na (7 Januari 2020m) imeandaa ratiba ya kuomboleza kifo cha mmbora wa wanawake duniani Swidiiqatul-Kubra Fatuma Zaharaa (a.s) –kwa mujibu wa riwaya ya pili- na kufanya majlisi ya kuomboleza ndani ya ukumbi wa utawala na kuhudhuriwa na watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) pamoja na mazuwaru, maombolezo hayo yataendelea kwa muda wa siku tatu.

Katika majlisi hiyo kulikua na mawaidha yaliyo tolewa na Shekh Aamir Jaburi, amezungumzia utukufu wa bibi Zaharaa (a.s), aidha amezungumzia dhulma alizo fanyiwa pamoja na namna alivyo pambana kwa aliji ya ujumbe wa Mwenyezi Mungu, vilevile akaeleza nafasi yake katika kujenga misingi ya uislamu na nguzo zake, Zaharaa (a.s) ni tunu kutoka kwa Mwenyezi Mungu na zawadi kwa Mtume (s.a.w.w) pia ni zaidi ya neema, ni siri ya maimamu watakasifu -maasumina- (a.s), akafafanua kua; uislamu umehifadhika hadi leo kwa utukufu na juhudi zake pamoja na kuwepo kwa Imamu wa mwisho Swahibu Zamaan Imamu Mahadi (a.f) ambaye ni baraka itokanayo na Swadiqah Twahirah (a.s).

Akamaliza mawaidha yake kwa kusoma kaswida iliyo eleza dhulma alizo fanyiwa bibi Zahara (a.s) na yaliyo jiri baada ya kifo cha baba yake (s.a.w.w).

Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya tukufu imeandaa ratiba ya maombolezo yenye vipengele vingi, kuna kipengele cha mawaidha na majlisi maalum za kuomboleza msiba huu, aidha imetangaza kua imejiandaa kupokea misafara ya waombolezaji kutoka ndani na nje ya mji wa Karbala, misafara inayokuja kumpa pole Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: