Atabatu Abbasiyya tukufu imewekwa mapambo meusi kufuatia kifo cha Swidiqatu Kubra Fatuma Zaharaa (a.s).

Maoni katika picha
Huzuni imetanda katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kufuatia kumbukumbu ya kifo cha mbora wa wanawake wa ulimwenguni Swidiqatu Kubra Fatuma Zaharaa (a.s) –kwa mujibu wa riwaya ya pili- kuta za Ataba tukufu na korido zake zimewekwa mapambo meusi na mabango yaliyo andikwa maneno ya kuomboleza kutokana na msiba huu mkubwa.

Kama kawaida Atabatu Abbasiyya tukufu imeandaa ratiba yenye vipengele vingi vya uombolezaji, ikiwa ni pamoja na utowaji wa mihadhara ya Dini pamoja na majlisi maalum za kuomboleza, sambamba na kujiandaa kupokea mawakibu za waombolezaji kutoka ndani na nje ya Karbala zinazo kuja kumpa pole Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).

Kumbuka kua msiba huu unaumiza sana nyoyo za waumini, huombolezwa na wafuasi wa Ahlulbait (a.s) kila sehemu ya dunia.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: