Baada ya kufunga sehemu zake muhimu: mlango wa kibla wa nje unakaribia kukamilika.

Maoni katika picha
Mafundi wa kitengo cha usimamizi wa kihandisi siku ya Jumatano (12 Jamadal-Uula 1441h) sawa na (8 Januari 2020m), wamemaliza kufunga sehemu muhimu za mlango wa kibla wan je kwenye Atabatu Abbasiyya, kwa hatua hiyo kitengo cha usimamizi wa kihandisi kinakaribia kumaliza uwekaji wa mlango huo.

Siku za nyumba rais wa kitengo cha usimamizi wa kihandisi, Mhandisi Samiri Abbasi aliongea kuhusu kazi hiyo kua: “mlango unao sogea ni matokeo ya usanifu wa kitengo cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu, umetengenezwa kwa ustadi mkubwa na umaridadi wa hali ya juu, mapambo na nakshi zake zinafanana na zile zilizopo katika milango mingine ya haram tukufu, ili kuweka hali ya uwiyano, kazi zote zimefanywa na mafundi wa kitengo chetu, tulianza kazi ya kuufunga mlango huu baada ya kukamilisha vipimo na vifaa vya lazima katika kazi hiyo”.

Akaongeza kua: Eneo la uzio wa geti linaupana wa mita (36) huku mlango wa geti ukiwa na upana wa mita (12) na urefu wa mita mbili, ni mlango mzuri, imara na unauwezo mkubwa wa kuvumilia harakati za mazuwaru, unawekwa kwa utaalamu wa hali ya juu, uzio wa geti na mlango huo kuna umbali wa mita (4) kufika kwenye lango kuu la Kibla.

Akafafanua kua: Kuhusu nakshi na mapambo yaliyopo kwenye uzio huo, yanatokana nay ale yaliyopo kwenye dirisha tukufu la malalo, kwa ajili ya kweka hali ya uwiyano wa kiufundi na kiujenzi kwenye haram takatifu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: