Idara ya ustawi wa jamii inaendelea kuzisaidia familia za mashahidi masikini na mayatima.

Maoni katika picha
Idara ya ustawi wa jamii chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu inaendelea kutoa misaada ya kibinadamu, kwa familia za mashahidi, masikini na mayatima, hivi karibuni tawi la Bagdad kitongoji cha Karkha limekwenda Diwaniyya wilaya ya Afak kutoa misaada.

Kiongozi wa idara ya Karkha ameongea kuhusu msafara huoa kua: Tumeandaa msafara chini ya anuani isemayo (kwa mfano huu wafanye kazi wenye kufanya), kupitia mawakibu zetu, kwa ajili ya kuzipa misaada familia za mashahidi, mayatima na masikini, kutegemea na mahitaji yao pamoja na kupunguza ugumu wa maisha.

Akaongeza kua: “Tumegawa nguo za watoto na vikapu vya chakula pamoja na hela na vitu vingine, tumefanya hayo kwa kushirikiana na idara ya mkoa wa Diwaniyya na tunashukuru kwa mapokezi mazuri tuliyo pata”.

Nazo familia zilizo nufaika na misaada hiyo zimeshukuru ukarimu wa idara ya ustawi wa jamii chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: