Kumbukumbu ya kifo cha Fatuma Zaharaa (a.s).

Maoni katika picha
Mwezi (13 Jamadal-Uula) ni siku aliyo ondoka duniani mmbora wa wanawake wa ulimwenguni na pande la nyama ya Mtume (s.a.w.w), mke wa kiongozi wa waumini (a.s) na mama wa maimamu watakasifu (a.s) Fatuma mtoto wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (a.s) kwa mujibu wa riwaya.

Katika siku kama ya leo mwaka wa (11) hijiriyya zilisikika sauti za vilio katika nyumba ya Ali (a.s), kisha mji mzima ukajaa vilio vya wanaume na wanawake, ikawa kama siku aliyo kufa Mtume (s.a.w.w), wanawake wa bani Hashim wakakusanyika katika nyumba ya Fatuma wakalia na kupaza sauti, watu wakaenda kwa Ali (a.s) wakamkuta amekaa katikati ya Hassan na Hussein wakiwa wanalia, Ummu Kulthum akawa anasema: Ewe baba yanyu, ewe Mtume wa Allah kwa hakika tumekukosa hatutakutana tena.

Watu wengi wakakusanyika huku wanalia wakisubiri jeneza litolewe ndani ili waliswalie, Abu Dhari akatoka na kusema: Ondokeni hakika mtoto wa Mtume hatatolewa muda huu.

Watu wakaondoka wanadhani kua jeneza litashindikizwa kesho asubuhi (imepokewa kua umauti ulimpata baada ya swala ya Alasiri au mwanzoni mwa usiku).

Imamu Ali (a.s) kwa kushirikiana na Asmaa alimuosha na kumvisha sanda usiku, kisha akaita: (ewe Hassan.. ewe Hussein.. ewe Zainabu.. ewe Ummu Kulthum njooni mmuone mama yenu, leo mnaagana mtakutana peponi), baada ya muda mfupi kiongozi wa waumini (a.s) akawaondoa.

Kisha Imamu Ali (a.s) akamswalia na akanyoosha mikono juu na kusema: (Ewe Mola huyu ni mtoto wa Mtume wako Fatuma, umemtoa katika giza na kumpeleka kwenye nuru, basi angazia maili na maili).

Baada ya kunyamaza sauti za watu na macho kulala, akatoka Kiongozi wa waumini pamoja na Abbasi, Fadhili na mtu wa nne wakiwa wamebeba jeneza hilo, huku wakishindikizwa na Hassan, Hussein, Aqiil, Saslamman, Abudhari, Mikdadi, Buraida na Ammaar.

Ali (a.s) akatelemka kaburini na kuupokea mwili wa pande la nyama ya Mtume (s.a.w.w), akamlaza kwenye mwana ndani halafu akasema: (ewe ardhi na namuweka kwako kipenzi wangu mtoto wa Mtume wa Mwenyezi Mungu, kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema mwenye kurehemu, bismillahi wa billahi wa ala millatu Rasulullahi Muhammad bun Abdillahi (s.a.w.w), ewe Swidiiqah nakukabidhi kwa aliye bora kwako zaidi yangu, nimekuridhia kwa yote aliyo kuridhia Mwenyezi Mungu), kisha akasoma aya isemayo: (Kutokana nayo (ardhi) tumekuumbeni, na humo tutakurudisheni, na kutoka humo tutakutoeni mara nyingine), halafu akatoka nje ya kaburi, waliokuwepo wakafukia kaburi kisha Ali (a.s) akalisawazisha kiasi ambacho halikujulikana lilipo chimbwa na halitajulikana hadi siku ya kiama.

Hivyo ndio alivyo ondoka Zaharaa (a.s) akiwa na hamu ya kukutana na Mola wake pamoja na baba yake, aliondoka akiwa na machungu makubwa, amekwenda kumshtakia Mwenyezi Mungu mtukufu atoe hukumu juu ya wale walio mdhulumu na kuchukua haki yake, amani iwe juu yake siku aliyo zaliwa na siku ailiyo uawa kishahidi na siku atakayo fufuliwa akiwa radhi mwenye kuridhiwa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: