Wajukuu wa Zaharaa (a.s) wanaomboleza kifo chake.

Maoni katika picha
Masayyid wanaofanya kazi katika Atabatu Abbasiyya tukufu wanaomboleza kifo cha bibi yao Zaharaa (a.s) kwa kufanya majlisi ya kuomboleza ndani ya haram ya kipenzi chake na kamanda wa jeshi la mwanae Abu Abdillahi Hussein na mbeba bendera wake Abulfadhil Abbasi (a.s).

Kwa mujibu wa maelezo ya kiongozi wa idara ya masayyid, Sayyid Hashim Shami amesema kua majlisi zitafanyika asubuhi ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa muda wa siku tatu, zinahudhuriwa na watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) pamoja na mazuwaru, kunakua na muhadhara kutoka kitendo cha Dini cha Atabatu Abbasiyya tukufu, ambayo itakua inatolewa na Shekh Ali Mujaan, anazungumza mada ya: (Itikadi yetu kuhusu bibi Zaharaa –a.s-), ndani ya siku hizi tatu atazungumzia mada hiyo pamoja na kueleza dhulma aliyo fanyiwa na utukufu aliokua nao mbele ya baba yake (s.a.w.w).

Akaendelea kusema: “Majlisi hizi zinafanywa chini ya idara ya maadhimisho ya kidini, ikiwa ni miongoni mwa matukio yaliyo umiza Maimamu wa Ahlulbait (a.s) ni hili tukio la kifo cha bibi Zaharaa (a.s)”.

Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya tukufu imeandaa ratiba maalum ya maombolezo haya, inahusisha kupokea waombolezaji na kuandaa majukwaa ya wazungumzaji wanao elezea matatizo aliyo pata bibi Fatuma Zaharaa (a.s) baada ya kifo cha baba yake Mtume (s.a.w.w).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: