Marjaa Dini mkuu: ushindani huongeza tatizo na huondoa uwezekano wa kulimaliza.

Maoni katika picha
Marjaa Dini mkuu amesisitiza kua kuamiliana kwa ushindani baina ya vikundi tofauti vyenye wafuasi na uwezo, kunaongeza tatizo na kuondoa uwezekano wa kulimaliza, akasema kua waathirika wakubwa ni wananchi wasiokua na uhusiano wowote katika vita ya ndani na ya nje inayo endelea.

Ameyasema hayo katika khutuba ya Ijumaa ya leo (14 Jamadal-Uula 1441h) sawa na (10 Januari 2020m) ndani ya haram ya Imamu Hussein (a.s), iliyo tolewa na Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, lifuatalo ni tamko kuhusu swala hilo.

(Hakika kuamiliana kwa pande tofauti zenye nguvu na wafuasi, na kila moja ikitaka kulazimisha maoni yake kwa kundi lingine, kutapelekea kukuza tatizo na kushindwa kupata muafaka, inawezekana makundi yote yakapata hasara, tena wananchi ndio waathirika wakubwa, hadi wale wasiokua na mchango katika vita ya ndani na nje inayo endelea, wala hawajihusishi na jambo lolote kuhusu amani ya taifa lao na utulivu, kwa kua na maisha bora kwao na kwa watoto wao).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: