Marjaa Dini mkuu: kuvunja heshima ya utawala wa Iraq na udhaifu wa serikali katika kulinda taifa ni sehemu ya matatizo yaliyopo.

Maoni katika picha
Marjaa Dini mkuu amesema kua yaliyo likumba taifa la Iraq siku chache zilizo pita, shambulizi na uvunjifu wa heshima kwa taifa, ni miongoni mwa matatizo ya sasa na udhaifu wa serikali katika kulinda taifa na raia, akamtaka kila mtu atafakari kama mambo haya yakiendelea hali itakuaje.

Lifuatalo ni tamko kuhusu swala hilo lililosomwa na mwakilishi wake Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi kwenye khutuba ya Ijumaa leo (14 Jamadal-Uula 1441h) sawa na (10 Januari 2020m) ndani ya haram ya Imamu Hussein (a.s).

(Yaliyotokea siku chache zilizo pita, shambulizi hatari na uvunjifu wa heshima ya taifa la Iraq, na udhaifu wa serikali katika kulinda taifa na raia wake, shambulio hilo na uvunjifu wa heshima, ni sehemu ya matatizo yanayo endelea, kila mtu anatakiwa atafakari hali itakuwa namna gani kama mambo haya yasipoisha, kila mtu akishikilia msimamo wake na akakataa kulegeza msimamo, bila shaka jambo hilo litasababisha matatizo kila sehemu, kwenye vyombo vya usalama, wanasiasa, uchumi na katika jamii, litatoa nafasi kwa watu wengine kuingilia mambo ya taifa letu na kutumia fursa hiyo kufanikisha mambo yao).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: