Marjaa Dini mkuu: dawa ya matatizo ya sasa ni kukubali kufanya mabadiliko (islahi).

Maoni katika picha
Marjaa Dini mkuu amesisitiza umuhimu wa kukubali madai ya mabadiliko (islahi) chini ya utaratibu ambao umesemwa mara nyingi, hiyo ndio dawa sahihi ya matatizo tuliyo nayo kwa sasa, akahimiza ulazima wa uzalendo na kuutafsiri kwa vitendo.

Amesema hayo katika khutuba ya Ijumaa leo (14 Jamadal-Uula 1441h) sawa na (10 Januari 2020m) ndani ya haram ya Imamu Hussein (a.s), iliyo somwa na Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, lifuatalo ni tamko kuhusu swala hilo:

(Kila mtu akiwa mzalendo na akiwajibika kwa taifa lake, akitafuta dawa ya matatizo tunayo pitia kwa sasa, akakubali kufanya mabadiliko yanayo takiwa chini ya utaratibu uliopangwa na kuzungumzwa mara nyingi, tutatoka salama kwenye matatizo haya kama tunataka kuyamaliza kwa njia inayo kubalika, baada ya kujitolea sana wananchi wa taifa hili katika maeneo mbalimbali).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: