Haya ndio maazimio ya kamati ya maandalizi katika kongamano la shahada la tisa.

Maoni katika picha
Kamati ya maandalizi ya kongamano la shahada la tisa, linalo simamiwa na chama cha Imamu Hussein (a.s) kwa kushirikiana na Ataba ya Alawiyya, Husseiniyya, Askariyya na Abbasiyya chini ya kauli mbiu isemayo: (Amani ya Fatuma –a.s- ni mwenendo wa wanaislahi) katika mtaa wa Dabuni mkoani Waasit, kamati imetoa maazimio mengi, miongoni mwa maazimio hayo ni:

  • 1- Kongamano hili linatokana na maelekezo ya Marjaa Dini mkuu na tunafuata muongozo wake katika kutumikia madhehebu ya Ahlulbait (a.s), tunatoa wito kwa kamati inayo ratibu kongamano ishikamane na misingi ya Fatwimiyya inayo wakilisha mafundisho ya Mtume (s.a.w.w), yaliyo lindwa na kufundishwa na Ahlulbait (a.s) kwa mujibu wa kauli ya Mtume (s.a.w.w) isemayo: (Nakuachieni vizito viwili kitabu cha Mwenyezi Mungu na kizazi cha watu wa nyumbani kwangu).
  • 2- Tunatoa wito wa kuheshimu matukio ya Dini yanayo huzunisha na kuacha kufanya sherehe au kufunga ndoa katika siku za matukio hayo.
  • 3- Tunatoa wito wa kuboresha kongamano na kuendelea kulitegemea na kushikamana na misingi yake, pamoja na kuunga mkono malengo yake, ukizingatia kua kongamano hili ni jukwaa ya kitamduni na kielimulimu, linafungua ukurasa wa uhusiano kati ya mtu na mazingira yanayo mzunguka chini ya nuru ya Ahlulbait na elimu yao sambamba na misingi ya kiislamu mitukufu.
  • 4- Tunatoa wito wa kuwajali vijana, kwani wao ndio wabeba bendera ya maendeleo, wanatakiwa wapambike kwa tabia za Ahlulbait (a.s).
  • 5- Tunatoa wito wa kuwajali wanawake, wao ndio msingi wa familia, kwani watoto hujifunza Zaidi kutoka kwao na wao ndio taifa la kesho na mustakbali wa taifa.
  • 6- Tunatoa wito wa kuunga mkono maonyesho ya vitabu kwani maonyesho hayo ni dirisha la utamaduni na njia ya kupanua fikra na kuongeza maarifa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: