Tukio la uchoraji wa watoto wenye umri chini ya miaka kumi ni miongoni mwa matukio muhimu katika kongamano la msimu wa huzuni za Fatwimiyya, linalo simamiwa na kitengo cha maadhimisho na mawakibu chini ya Ataba mbili tukufu kila mwaka kwenye uwanja wa katikati ya haram mbili, zowezi hilo husimamiwa na kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya kupitia wanafunzi wake wenye umri mdogo.
Kuhusu jambo hilo tumeongea na rais wa kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya Dokta Ahmadi Kaábi amesema kua: “Shule za Al-Ameed chini ya kamati ya malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, zimezowea kufanya jambo hilo kila wakati wa kongamano la msimu wa huzuni za Fatwimiyya kwa kutumia wanafunzi wenye umri mdogo, kila mwaka huitwa kundi la wanafunzi wenye umri chini ya miaka kumi, na hupewa nafasi ya kuchora tukio lililo pelekea shahada ya Swidiqah Twahirah Fatuma Zaharaa (a.s)”.
Akaongeza kua: “Lengo la kufanya hivyo ni kuingiza mapenzi ya Ahlulbait (a.s) katika nafsi zao, na kuwajulisha madhila na dhulma walizo fanyiwa, kupitia fani ya uchoraji ambayo hugusa hisia za roho”.
Kumbuka kua kitengo cha maadhimisho na mawakibu chini ya Ataba mbili tukufu, hivi karibuni imefanya awamu ya kumi na tatu ya kongamano la msimu wa huzuni za Fatwimiyya, ambalo shughuli zake hufanyiwa katika uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu.