Tangazo: kitengo cha malezi na elimu ya juu kimetangaza haja ya kufanya makubaliano na walimu.

Maoni katika picha
Kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimeonyesha umuhimu wa kufanya makubaliano maalum na walimu wenye vyeti vya (diploma, bachela, masta na dokta), wanaofanya kazi katika shule za Al-Ameed.

Walimu hao wawasili katika shule za Al-Ameed zilizopo mtaa wa Baladiyya barabara ya Nahri karibu na maduka ya Haji Raádu Shuuk, kuanzia Jumamosi ya tarehe (18/01/2020m).

Kwanza: Mambo yanayo hitajika:

  • 1- Kufundisha somo ulilo bobea.
  • 2- Kuwasilisha daftari la andalio la somo.
  • 3- Kuwasilisha vifaa vya kufundishia, na inapendekezwa viwe vya kisasa.
  • 4- Kuwasilisha vielelezo vinne au kitambulisho cha taifa pamoja na uthibitisho wa kuhitimu masomo yako (cheti).

Pili: Maelezo mengine:

  • Maandalizi ya jaribio.
  • Kuwasilisha faili lenye (barua ya maombi, kopi za rangi za vielelezo vinne, kopi ya cheti ya rangi, vielelezo vyovyote vinavyo thibitisha elimu yako).
  • Muombaji awe ni mkazi wa Karbala.

Tatu: Masomo yanayo hitajika:

(Masomo ya tarbiyya na saikolojia), waombaji wawe ni wahitimu wa chuo cha (sayansi na adabu) na wahitimu wa chuo cha misingi ya malezi au wahitimu wa maahadi za kuandaa walimu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: