Katika muendelezo wa maombolezo yaliyo ratibiwa na Atabatu Abbasiyya kutokana na kifo cha pande la nyama ya Mtume (s.a.w.w) na mke wa Murtadha (a.s) bibi Swidiqah Kubra Fatuma Zaharaa (a.s), idara ya wahadhiri wa Husseiniyya wa kike chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu imeandaa majlisi ya kuomboleza ambayo wameshiriki kundi kubwa la mazuwaru, ndani ya haram ya kipenzi wake Abulfadhil Abbasi (a.s) ndani ya Sardabu ya Imamu Jawaad (a.s).
Majlis hiyo imehusisha muhadhara kuhusu utukufu wa bibi Fatuma (a.s) na nafasi yake mbele ya Mwenyezi Mungu mtukufu, ikabainishwa kua bibi Fatuma Zaharaa (a.s) ni mfano bora kwa mwanamke muumini, kwa kila mwanamke anatakiwa atambue jukumu la kuendeleza jamii na kupambana na changamoto mbalimbali za kifikra, katika kufanya hivyo anatakiwa kumtanguliza na kumuiga bibi Fatuma Zaharaa (a.s), ikahimizwa kusoma na kusomesha pamoja na kuheshimu mwalimu, akatambulishwa bibi Fatuma Zaharaa (a.s) na namna ya kumfuata.
Kulikua na vipengele vingine vya kuomboleza ikiwa ni pamoja na kaswida mbalimbali kuhusu msiba huo, mwisho wa majlis hiyo watu wote walinyanyua mikono juu na kumuomba Mwenyezi Mungu aharakishe faraja ya Swahibu Asri wa Zamaan (a.f) na ainusuru Iraq na raia wake pamoja na miji yote ya kiislamu.