Kufunga semina ya uhakiki wa nakalakale (makhtuutu) na faharasi

Maoni katika picha
Miongoni mwa mfululizo wa semina za kitaalamu, hivi karibuni kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia kituo cha turathi za kusini kilicho chini yake kimehitimisha semina kuhusu uhakiki wa nakalakale (makhtuutu) na faharasi, ambayo ilikua na zaidi ya washiriki ishirini pamoja na wanafunzi wa Dini na watumishi wa kituo, lengo la semina ni kuonyesha umuhimu wa kufanya uhakiki wa nakalakale na faharasi kwa undani.

Semina ilikua ya siku kumi chini ya ukufunzi wa Shekh Mahmuud Duryabi Najafi ambaye amesema kua: “Lengo la semina hii ni kuandaa wataalam wenye uwezo wa kuhakiki nakalakale na vitabu, kisha kuviandika katika muonekano mpya”.

Washiriki wa semina wamesema kua wamejifunza mambo mengi miongoni mwa taratibu za kufanya uhakiki, kupitia mijadala mbalimbali waliyokua wakifanya wakati wa semina hiyo baina yao na wakufunzi, wanaweza kufika katika lengo lao la kuimarisha misingi ya elimu hii, wametoa shukrani nyingi kwa kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu kwa kuwapa fursa hii adhim, na wakakitakia mafanikio mema kituo hiki.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: