Makamo katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu Ustadh Maitham Zaidi amepongeza kazi iliyofanywa na kikosi cha Rahmatul-Insaniyya chini ya ustawi wa jamii katika mkoa wa Muthanna, katika kipindi ambacho kilikua na kazi nyingi.
Yamesemwa hayo katika ziara iliyofanywa na kikosi hicho pamoja na kiongozi wa idara ya ustawi wa jamii chini ya Atabatu Abbasiyya Shekh Abbasi Akaishi.
Wamejadiliana kuhusu shughuli zinazo fanywa na kikosi hicho kwa ujumla, Zaidi ameeleza shughuli zilizo fanywa na idara hiyo, na matokeo ya shughuli hizo kwa kushirikiana na idara ya ustawi wa jamii ya Atabatu Abbasiyya tukufu.
Mwishoni mwa mazungumzo yao makamo katibu mkuu akasifu kazi zinazo fanywa na idara hiyo kupitia matawi yake yanayo shirikiana kwa karibu na mawakibu za kutoa misaada pamoja na vikundi vingine vya kujitolea, kikiwemo kikundi cha Rahmatul-Insaniyya, pia akawafikishia shukrani na pongezi kutoka kwa kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu, na akawaombea baraka na mafanikio katika shughuli zao.