Nadwa kuhusu mwenendo wa bibi Zaharaa (a.s).

Maoni katika picha
Kwa machungu na huzuni kubwa kufuatia kumbukumbu ya kifo cha bibi Zaharaa (a.s), miongoni mwa ratiba za ofisi ya wanawake ni (Zakiyaatu Twayyibaatu) ya kuhuisha kumbukumbu ya Ahlulbait (a.s) katika matukio mbalimbali, wamefanya nadwa ya kujadili mafundisho yanayopatikana katika khutuba ya Fadakiyya ya bibi Zaharaa (a.s), ili wanawake waige kutoka kwake namna ya kufanya harakati na kupambana na uovu katika jamii.

Bibi Asmaa Abadi kiongozi wa ofisi ya wanawake amesema kua: Idara ya wanawake inazingatia kuhuisha mambo ya Ahlulbait (a.s) katika kuadhimisha matukio yao kwa kufanya mambo tofauti, ili wabakie milele katika akili za watu, upekee wa nadwa hii ni kutoa nafasi ya kujadiliana kwa uwazi, jambo ambalo linasaidia kukazia maarifa mada inayo wasilishwa kitafiti na kwa hoja sahihi.

Akamaliza kwa kusema: Matukio ya kidini ni fursa kubwa na yanamchango muhimu katika kuzielewa turathi za umma, kuzihuisha na kuzifanya ziendelee kuwepo kwa wanaadamu, ufanyaji wa nadwa hizi ni njia ya kudumisha turathi hizo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: